Home » » Mil. 65/- kukamilisha ujenzi Hospitali Ngamiani

Mil. 65/- kukamilisha ujenzi Hospitali Ngamiani

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imetenga sh milioni 65 kukamilisha ujenzi  wa jengo la kliniki, wodi ya watoto na stoo ya dawa katika Hospitali ya Ngamiani.
Diwani wa Majengo, Mohamed Jeff, alibainisha hayo jana alipozungunza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo na kueleza maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2009 hadi 2014.
Alisema pamoja na hatua hiyo, pia halmashauri imekamilisha majengo mengine kama vile jengo la ushauri nasaha na upimaji wa ukimwi pamoja na jengo la wagonjwa wa kifua kikuu (TB).

Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa