Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAKAZI wa kaya 30 wa mitaa ya Majanimapana na Nguvumali
zinazotarajiwa kubomolewa makazi yao kupisha ujenzi wa barabara
zimetangaza mgogoro na serikali kwa kugoma kuhama na kumtaka Rais
Jakaya Kikwete kuingilia kati.
Kwa mujibu wa kamati ya wahanga hao wameiomba serikali kupitisha
barabara hiyo maarufu ‘barabara ya Museveni’ inayotokea Kenya, Tanzania
na Uganda maeneo ya Mabanda ya Papa ilikokuwa imepangiwa awali au
sehemu za Idara ya Ndorobo ambako hakuna makazi ya watu.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Salimu Mbughuni, alisema wakazi hao
wanaitaka serikali kubadilisha muelekeo wa mradi huo na kwamba wao
hawapo tayari kuhama wala kupokea fidia.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment