Home » » Diwani, Mtendaji wanusurika kuchomwa moto

Diwani, Mtendaji wanusurika kuchomwa moto

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
DIWANI wa Isakamaliwa, Igunga, Doto Kwilasa, Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Erasto Shokoro, wajumbe sita wa serikali ya kijiji na mtu ambaye hajajulikana wamenusurika kuchomwa moto na wananchi.
Wananchi hao waliwafungia ndani ya chumba cha mikutano viongozi hao kwa madai ya kuitisha kikao cha kuwazuia vijana wa Isakamaliwa wasilipize kisasi kwa wafugaji waliowachoma mikuki vijana wenzao.
Vurugu za kutaka kuchoma moto chumba hicho zilitokea juzi katika Kijiji cha Isakamaliwa baada ya makundi mawili ya wafugaji wa kata hiyo kutofautiana na kusababisha kundi moja kushambulia jingine kwa mikuki wakidaiwa kuingiza mifugo kinyume cha sheria katika bonde la Magogo.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa