Home » » AUA KIKONGWE ,NAYE AUAWA

AUA KIKONGWE ,NAYE AUAWA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Kilindi. Kijana mmoja mkazi wa Kijiji cha Mabalanga wilayani Kilindi, Hassani Said (28) amemuua kwa kumkata na jembe kichwani bibi yake, lakini baadaye akauawa na wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili, mkazi mmoja wa kijiji hicho Omari Waziri alisema kuwa Februari 25 mwaka huu kijana huyo alikuwa akitoka shamba na bibi yake aliyefahamika kwa jina la Mwajuma Waziri (62), lakini ghafla alinyanyua jembe alilobeba na kumkata kichwani bibi yake na kufariki dunia.
Alisema kuwa baada ya kufanya mauaji hayo, Hassan alijificha kwenye nyumba iliyo jirani na wananchi walipopata taarifa akiwemo babu yake, Mkomwa Mkombozi (72) walikwenda kwa lengo la kumkamata.
Katika jitihada za kumkamata, mtuhumiwa alitoa panga na kumjeruhi vibaya Mkombozi ambaye anaendelea kupata matibabu kwenye Hospitali ya Handeni.
Baada ya kumtia mikononi, wananchi walimshambulia kwa zana mbalimbali hadi kumuua.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa, mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe alipotafutwa na kuhusu tukio hilo, alisema hafahamu lolote kwa vile yuko nje ya ofisi.
 Chanzo;Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa