Home » » Wakazi walazimika kula mizizi

Wakazi walazimika kula mizizi

WAKAZI wa Kata za Mashewa na Mkomazi, wilayani Korogwe, mkoani Tanga wamelazimika kula mizizi ya miti na matunda ili kunusuru maisha yao
kutokana na kukabiliwa na baa la njaa.
Kufuatia hali hiyo, wananchi hao wameiomba serikali kupeleka chakula
cha msaada haraka kwa vijiji hivyo vilivyoathiriwa na tatizo hilo ili
kuokoa maisha yao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtonibombo, Kata ya Mashewa, Nuru Tina,
alithibitisha kutokea kwa hali hiyo ambapo wananchi wamekuwa
wakishindwa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo kutoka na ukosefu
wa chakula.
“Ukosefu wa mvua za uhakika umesababisha kukosekana kwa chakula kwani mahindi yaliyopandwa yote yamekauka kutokana na ukame uliosababishwa na mvua kushindwa kunyesha kwa wakati na kuwa chache,” alisema
Tina.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Kulasi, Kata ya Mashewa, Teresia Ngonyani,
alisema msaada wa haraka unahitajika kunusuru maisha ya wakazi hao.
Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mrisho Gambo, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuwa halmashauri wa wilaya hiyo inafanya tathmini ya vijiji vilivyoathirika kwa ajili ya kupatiwa msaada.
Tayari wilaya hiyo imegawiwa zaidi ya tani 35 za chakula kiasi ambacho
ofisa kilimo na chakula wa halmashauri hiyo alikaririwa na gazeti hili akisema kuwa msaada huo hauwezi kukidhi mahitaji ya wakazi hao.
Chanzo;Mwananchi

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa