JUMLA ya vikundi vya Vicoba 170 vyenye thamani ya zaidi ya sh
milioni 600 vimeanzishwa wilayani hapa kuanzia mwaka 2005 hadi 2009.
Mratibu wa Vicoba Wilaya ya Lushoto, Hande Mwanjela, alieleza hayo
alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya Vicoba wilayani hapa na kusema
kuwa walianza na vikundi 16 mwaka 2005.
Alisema wakati wote wa uhamasishaji wa uanzishwaji wa vikundi hivyo,
wanachama ndio waliopewa jukumu la kuwalipa wawezeshaji, na kwamba
ushirikiano huo na wataalamu umesababisha maendeleo makubwa kwenye
vikundi hivyo.
Mkufunzi wa Vicoba, Ayub Russia, alisema kuwa kikundi cha Mwongozo
ambacho wanachama wake wanapata vyeti, ni miongoni mwa vikundi 25
vilivyomo katika Tarafa ya Mlalo ambavyo vina wanachama 754.
Alisema miongoni mwa changamoto za vikundi hivyo mbali na tatizo la
mitaji, ni itikadi za kidini na wanasiasa ambao wamekuwa wakitoa
tafsiri zisizo sahihi kuhusu maana na dhana halisi ya Vicoba.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment