Home » » MGAMBO JKT YAPANIA KUTOSHUKA DARAJA

MGAMBO JKT YAPANIA KUTOSHUKA DARAJA

TIMU ya Mgambo JKT imejipanga kuhakikisha haishuki daraja msimu huu na inafanya kila jitihada kufikia lengo lake hilo.

Akizungumza baada ya mchezo baina ya Timu yake na wenyeji Rhino rangers kocha wa Mgambo JKT, Bakari Shime, amesema wamejipanga msimu huu wasiteremke daraja huku akiwapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kufuata maelekezo yake.

Naye Kocha wa Rhino Rangers, Jumanne Chale, mbali ya kuitupia lawama safu yake ya ulinzi, amesema bado hawajakata tamaa na wanapambana kuhakikisha wanafanya vizuri msimu huu

Kwenye mchezo uliochezwa jana katika uwanja wa Ali Haasan Mwinyi Mjini Tabora, Timu hizo zilitoka sare ya kufungana bao moja moja

Mchezo huo ni wa tatu mfululizo kwa Timu ya Rhino rangers kwenye uwanja wa nyumbani wa Ali Hassan Mwinyi na kuambulia pointi mbili tu baada ya kutoka sare michezo miwili na mmoja kupoteza


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa