Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KAMANDA wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini
(Takukuru) Mkoa wa Tanga, Edson Makallo, amesema sheria ya kulinda siri
za mteja inayotumika katika taasisi za fedha ni kikwazo kwa vyombo vya
upelelezi vinavyochunguza makosa ya mapapa wanaotorosha fedha nje ya
nchi.
Makallo alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi wakati akifungua mafunzo ya
wiki moja ya wakaguzi wa ndani wa Hesabu za Serikali inayofanyika
Hoteli ya Mkonge.
Alisema vyombo vya upelelezi vinakumbana na vikwazo vya sheria
inayotumiwa na taasisi za fedha ya kulinda siri ya mteja na kwamba
mapapa wanaotorosha fedha nje ya nchi wamekuwa wakikwepa kuchunguzwa
kupitia sheria hiyo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment