Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAFUGAJI wa Kata ya Kwamatuku, Wilaya ya Handeni, mkoani
Tanga, wamemlalamikia diwani wa kata hiyo, Mustaph Beleko, kuwa
anatumia vibaya agizo la Mkuu wa Wilaya hiyo, Muhingo Rweyemamu la
kupunguza mifugo kwa kuendesha zoezi hilo kwa upendeleo.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wafugaji hao walisema
diwani huyo ameegemea upande wa wakulima kwa lengo la kujijenga kisiasa
kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Nosa Irurai, alieleza hali hiyo inaashiria mgogoro mkubwa na
kwamba wafugaji hao wanadai kuchoshwa na matukio ya kikatili kwao
na mifugo yao kwa madai kuwa wanalipishwa faini ya kati ya sh 150,000
hadi 300,000 bila vikao vya kisheria.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment