Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MVUA iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo ikiambatana na kimbunga,
imeangusha nguzo 35 za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na
kusababisha ukosefu wa umeme kwa wilaya za Handeni na Kilindi, mkoani
Tanga.
Mvua hiyo kubwa ambayo haijapata kutokea kwa miaka 10, imesababisha
mafuriko kwenye vijiji vya Kwamsala, Sindeni na Misima, Handeni na
kuacha hofu ya kurudi tena kwa kimbunga hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye Kijiji cha Misima
juzi, Meneja wa TANESCO Handeni, Emmanuel Mossy, alisema kimbunga
hicho kimeisababishia hasara kwa shirika na wateja wake na kwamba
haijulikani huduma ya umeme itarejea lini.
Alisema jitihada ambazo shirika hilo linazifanya ni kurejesha haraka
huduma ya umeme kwa kuweka nguzo mpya baada ya awali kung’olewa na
baadhi kukatika, hivyo kuwataka wateja wake kuwa wavumilivu wakati
shirika hilo likijitahidi kuirejesha huduma hiyo.
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment