Korogwe ; Watu watano wanaodhaniwa kuwa
majambazi wamekamatwa na polisi wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa tuhuma
za kukutwa na bunduki aina ya Shortgun na sare za polisi wakati
wakijiandaa kwenda kufanya uhalifu .
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa Polisi mkoani
Tanga, Costantine Massawe alisema majambazi hao wamekamatwa Kijiji cha
Gomba Kata ya Makuyuni wilayani hapa Desemba 28 mwaka huu saa 4:00 usiku
baada ya kupata taarifa kutoka kwa msamaria mwema .
Kamanda Massawe alisema bunduki hiyo iliyokuwa na
risasi tatu, ina namba ya Model-1400 MK II ambayo Taratibu Hemed ndiye
anayeimiliki kihalali, lakini amekuwa akiikodisha kwa majambazi na
kuletewa fedha anazotumia kulipia kibali cha silaha hiyo.
Massawe aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Zacharia
Jeras {50] Mkazi wa Makanya Same Kilimanjaro , Mosses Jonasi {44} na
Selemani Jaha {21} wote wakiwa wakazi wa Makanya Same mkoani Kilimanjaro
ambapo walikiri kwenda kufanya uhalifu katika kijiji hicho cha Gomba.
Alitaja watuhumiwa wengine kuwa ni Taratibu
Hemedi{74} ambaye ni mmiliki wa silaha hizo na sare pamoja na Hemedi
Taratibu {32} ambaye ni mtoto wa mtuhumiwa anayemiliki silaha hizo na
sare hizo ambazo ni za polisi.
Kamanda huyo alisema polisi inaendelea na uchunguzi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment