Idadi
ya watu waliokufa katika ajali ya basi la Burdani iliyotokea wiki
iliyopita, imeongezeka na kufikia 16 baada ya abiria wanne kufariki
dunia.
Basi hilo lilikuwa likitoka Wilaya ya Korogwe, mkoani Tanga, kwenda Dar es Salaam na lilipata ajali katika Kijiji cha Taula, Kata ya Kwedizinga, wilayani Handeni, saa moja asubuhi na kuua watu 12.
Akizungumza
na Majira jana, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga, wilayani
Korogwe, Dkt. Edes John, alisema watu wawili walifariki katika
Hospitali ya Bombo wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.
Aliwataja
watu hao kuwa ni Said Mohamed, mkazi wa Bumbuli wilayani Lushoto na
Isack Mbwambo, mkazi wa Korogwe Mjini ambaye ni mtoto wa mwaka mmoja na
nusu.
Alisema mmoja alifariki katika Hospitali ya KCMC iliyopo Mjini
Moshi, mkoani Kilimanjaro ambaye ni Athuman Said (aliyekuwa kondakta)
na Rahma Abdul alifariki katika Hospitali ya Magunga, wote wakazi wa
Korogwe.
“Hadi sasa, katika Hospitali ya Magunga wamelazwa wanawake
kumi na mwanaume mmoja, KCMC walipelekwa majeruhi 10, Bombo mmoja,
waliofariki Hospitali ya Bombo hawakupitia Magunga, walichukuliwa moja
kwa moja eneo la ajali.
“Hospitali ya Taifa Muhimbili walipelekwa
majeruhi watano akiwemo mdogo wake na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Joel
Bendera ambaye ni Francis Bendera,” alisema
Chanzo;Mtanzania
0 comments:
Post a Comment