Tanga. Abiria sita wamekufa papo hapo na
wengine 21 kujeruhiwa baada yabasi dogo walilokuwa wakisafiria maarufu
kama daladala kugongana usokwa uso na lori aina ya Volvo katika eneo la
Kange kwenye Barabara Kuu ya Tanga kwenda Segera.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na
kuthibitishwa na Kamanda waPolisi Mkoa wa Tanga,Costantine Massawe ni
kuwa ajali hiyo ilitokeausiku wa kuamkia jana Jumapili saa 2.30 usiku
ambapo Hiace hiyoilikuwa ikitokea Tanga mjini kuelekea kitongoni cha
Kange kilichokonje ya mji. Ajali hiyo ambayo imewashtua wakazi wa Jiji
la Tanga ilihusisha Hiaceiliyokuwa ikiendeshwa na Gadiel Wilkael (44)
ambaye pia ndiye mmlikialiyekufa papo hapo na Volvo yenye tela iliyokuwa
imeegeshwabarabarani.
Waliokufa katika ajali hiyo kwa mujibu wa Massawe
ni pamoja na derevawa Hiace ambaye pia ni mmiliki wa daladala hiyo
Gabriel Wilkaeli (44) Raymond Mapunda (28), Halima Shaka(28), Mary
Chilongoi (37) GloriaKidenya (1), Femida John (38) ambapo miili hiyo
imeshatambuliwa na ndugu zao.
Alisema majeruhi katika ajali hiyo walikimbizwa katika Hospitali yaMkoa wa Tanga ya Bombo kwa ajili ya matibabu.
Muuguzi wa zamu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Tanga ya Bombo,Alice Mnkande aliifahamisha Mwananchi kuwa usiku huo
walipokea miiliya marehemu sita na majeruhi 21 waliotokana na ajali hiyo
ya Hiace.
Kamanda Massawe alisema chanzo cha ajali hiyo ni
dereva wa Hiace hiyokutaka kupita gari nyingine ambapo alikutana na
gari nyingine mbelena ndipo aliporudi ili kukwepa na akakutana Lori hilo
lililokuwa mbeleyake.
“Dereva wa Hiace alitaka “ku-overtake” gari
nyingine ndipo alipokutanana gari mbele yake, sasa ili arudi kwenye
mstari akashindwa na matokeo yake akagongana uso kwa uso na hili lori ”,
alisema.Alisema kati ya majeruhi hao 21 waliotibiwa na kurudi nyumbani
ni sita wanawake wawili na wanaume wanne na kwamba 15 bado wapo wodini
wakiendelea na matibabu.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment