WAKULIMA mpunga wa Skimu ya Mahenge, wilayani Korogwe wamepewa mkopo wa
Sh milioni 80 na Benki ya CRDB, kwa ajili ya kuinua kilimo cha mpunga.
Hayo yamesema jana na Diwani wa Kata ya Kwamdolwa, Hillar Ngonyani
(CCM), alipokuwa akitoa taarifa yake utekelezaji wa miradi ya maendeleo
kwa kipindi cha miezi mitatu.
Alisema kuwa fedha hizo zimetokana na andiko lililowasilishwa na Chama cha Ushirika cha Kumekucha kwa kushirikiana na Manundu SACCOS, ambapo walifanikiwa kupata fedha hizo kupitia benki ya CRDB.
“Mheshimiwa Mwenyekiti tunaomba tujipongeze hapa mbele ya Benki ya CRDB kwa kuwapatia wakulima wetu 160 mkopo, ambao utawasaidia kuleta tija katika kilimo cha mpunga kwa wakulima wetu wa Skimu ya mahenge,” alisema Ngonyani.
Pamoja na hatua hiyo diwani huyo alisema kuwa skimu hiyo iliyokuwa na jumla wakulima wapatao 360, 160 ndio walionufaika kwa kupata mkopo na wengine 200 wanatarajiwa kupata mkopo mwingine baada ya hatua za awali za mafunzo ya jinsi ya utunzaji fedha za mikopo kukamilika.

CHANZO;MTANZANIA
0 comments:
Post a Comment