Home » » Chanzo cha umaskini chabainishwa

Chanzo cha umaskini chabainishwa



IMEELEZWA  kuwa chanzo  cha umaskini nchini ni mahusiano mabaya kati ya viongozi wa kuchaguliwa na wananchi  wa maeneo husika.
 Wakiuzungumzia  kwa nyakati  tofauti  wakati  wa mahojiano na gazeti hili  baadhi ya wananchi ambao ni wakazi wa vijiji mbalimbali  wilayani hapa,  walieleza kuwa viongozi ndio tatizo na chimbuko la kudumu kwa maendeleo nchini.
Mmoja wa wananchi  hao, Sadick Ramadhan, alisema viongozi wanaodumaza maendeleo ni wale walioingia madarakani kwa mizengwe wakiwa na lengo la kujinufaisha badala ya kuwanufaisha wananchi waliompa ridhaa ya kuwaongoza.
Naye  Nassoro Mojera alisema rushwa katika uchaguzi, ndiyo tatizo la viongozi wanaotangazwa  na tume ambao si chaguo la wananchi.
Mojera aliongeza kuwa kutokana na viongozi kupatikana kwa njia ya rushwa na kutokuwa na ridhaa ya wananchi ni vigumu kujenga mahusiano ambayo yangewawezesha kukaa pamoja na kujadili maendeleo yao.
Yassin Kabelwa  yeye alieleza sababu mbalimbali zinazochangia kuvunjika kwa mahusiano baina ya viongozi na wananchi na kuzitaja baadhi kuwa ni ubinafsi wa viongozi, na ushabiki wakati wa uchaguzi.

CHANZO;TANZANIA DAIMA

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa