Zaidi ya wanawake 30 wakiwa na watoto wao wamekataliwa
na jamii zao kwa kuhofiwa kuwa wanaweza kusababisha tena maafa kama
yaliyojitokeza katika kijiji cha Lulago, kata ya Lwande wilayani Kilindi
yaliyosababisha kifo cha askari Mgambo wa kijiji cha Lwande, Salum Mgonje na
kujeruhiwa kwa risasi Mkuu wa Kituo cha Polisi Kilindi Lusekelo Edward.
Wanawake hao ambao wamehifadhiwa katika kambi maalum kwenye makao makuu ya wilaya ya Kilindi ya Songechini iliyowekwa chini ya ulinzi mkali wa polisi, waliolewa na watu wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya askari mgambo huyo pamoja na kumjeruhi Inspekta Edward na kisha kukimbilia msituni na kuwatelekeza.
NIPASHE jana lilifika katika vijiji vya Lwande na Lulago na kuzungumza na wananchi wa vijiji hivyo, ambao wengi walilalamika kuchoshwa na unyanyasaji na watu wanaounda kundi lililofanya uhalifu huo.
“Jamani sisi tunasema japo kuwa wanawake hao ni watoto wetu hapa kijijini lakini watakuwa wamerithi tu roho za waume zao sasa wabaki huko huko na ikibidi mkuu wa mkoa akawajengee nyumba Tanga huku hatuwataki wametunyanyasa sana tumechoka nao…kila siku sisi ni wa kupigwa mapanga na kuchapwa viboko kisa tumewasha redio kwa nguvu jamani kweli,” alisema Athman Bakari (60) mkazi wa kijiji cha Lwande.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Lwande Salim Mangole alisema watu hao waliingia kijijini hapo mwaka 2008 wakitokea jijini Dar es Salaam wakiwa katika gari aina ya Coaster iliyokuwa na kibao mbele cha Mbagala-Temeke na kupokelewa na mwenyeji wao mkazi wa kijiji hicho.
Alisema baada ya kuingia kijijini hapo bila kufuata taratibu, serikali ya kijiji ilimwandikia barua mwenyeji wao huyo (anamtaja jina) na kumtaka kuwatambulisha rasmi wageni wake kwa uongozi wa kijiji jambo ambalo walilipinga na kusema kuwa hawaitambui serikali bali Mungu tu.
Alisema watu hao walijitengea eneo maalum karibu na kijiji ambapo hakuna mwanakijiji aliyekuwa akiruhusiwa kupita katika eneo hilo na kwamba walifanya vitendo mbalimbali vya kihalifu ikiwemo kuwapiga wananchi na watoto waliokuwa wakisoma shule za msingi kwa madai kuwa walitakiwa kusoma madrasa badala ya shule za serikali.
“Kuna siku kijana mmoja alikuwa anaendesha Bodaboda huku inalia mziki basi walimkamata wakampiga kwa mapanga walipoitwa na serikali ya kijiji walikataa kama kawaida na tuliripoti polisi lakini hata polisi waliwajibu kuwa hawaitambui serikali bali Mungu na hivyo hivyo watoto wa shule wakipita wanawapiga na kuwalazimisha kuingia kwenye madrasa zao ambazo wanawafundisha namna ya kupigana na kuua,” alisema Mwenyekiti huyo wa kijiji.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Lwande Mwanaisha Sindege alisema wananchi wa maeneo hayo walishatoa malalamiko yao mara kwa mara kwa polisi kutokana na vitendo vya unyanyasaji vilivyokuwa vikifanywa na watu hao.
Alisema watu hao walikuwa na kiongozi wao waliyekuwa wakimwita kwa jina la Masta ambaye ndiye aliyekuwa akitoa msimamo wa kila jambo wanalolifanya.
“Sasa siku ile ya tukio wakati polisi wakimtafuta Masta ndipo wananchi wenye hasira kali walipowasha moto kambi ya wale watu na kuanza kuwatafuta kwenye mapori,” alisema Afisa Mtendaji Kata huyo.
Kwa mujibu wa Sindege, baadhi ya watu hao wana asili ya Somalia na kwamba walijigawa kwa makundi tofauti tofauti ikiwamo mkuu wa kitengo cha kungfu na mkuu wa kitengo cha visu.
Mpaka sasa watu 44 wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa wakiwa na silaha mbalimbali za moto na za jadi ikiwamo bastola mbili, shortgun moja, magobole matatu, mapanga 18, shoka mbili, visu 10, baruti, na nguo zinazoaminika kuwa ni za kijeshi.

CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment