Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, amesema watu waliomuua
askari mgambo Salum Mgonje na kumpiga risasi Mkuu wa Kituo cha Polisi
Songe, wilayani Kilindi Edward Lusekolo ni kikundi kilichokuwa kinaishi
msituni.
![]() |
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa |
Alisema kikundi hicho kinaipinga Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na kudai ni ya kikafiri kikiwa na mipango ya kutaka Tanzania isitawalike.Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Handeni, Bi. Gallawa alisema kikundi hicho kiliweka kambi tatu wilayani humo kikifanya mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kijeshi.
“Pia
kikundi hiki ndicho kilichokuwa kikipinga mchakato wa sensa mwaka 2012,
kambi zao tatu zilikuwa katika Kata ya Lwande na Negero kwenye Kijiji
cha Madina.“Katika kambi ya Madina, wafuasi wao wawili wameuawa
baada ya kupinga kitendo cha kukamatwa na askari Oktoba 26 mwaka huu
wakijiita wafuasi wa Sunni,” alisema.
Aliwataja
wafuasi waliouawa kuwa ni Ramadhan Hamis, ambaye ni mfanyabiashara wa
madini na mwingine jina lake halikufahamika mara moja lakini inasemekana
ni mwalimu wa dini ya Kiislamu (ustaadh) Kijiji cha Lwande.
Aliongeza
kuwa, kikundi hicho kimekutwa na bunduki tatu aina ya gobore, shortgun
moja, bastola mbili zilizotengenezwa kienyeji, mapanga 18 na visu 10.
Bi. Gallawa alisema wafuasi 46 wa kikundi hicho tayari wamekamatwa
lakini jambo la kushangaza wamo watumishi wa Serikali ambao ni walimu wa
shule za msingi na watafikishwa mahakamani wakati wowote.
Kamati
ya Ulinzi na Usalama Mkoa, ambayo inaongozwa na Bi. Gallawa, imeamua
kuweka kambi Kilindi kwani hivi sasa hali ya usalama si nzuri hadi
itakapotulia. Akizungumza na
Majira hivi karibuni, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Constantine Masawe,
alisema askari mgambo Salum Mgonje aliuawa Oktoba 22 mwaka huu ambapo
Edward alipigwa risasi za mbavu na mkononi Oktoba 23, saa mbili usiku.
Kikundi
hicho kinajumuisha wakazi wa vijiji mbalimbali wilayani humo ambao
wamefukuzwa na wenzao kutokana na tabia zao za kupinga mambo mbalimbali
ya maendeleo. Chanzo cha
kuanzishwa kikundi hicho ni baada ya mwenzao mmoja ambaye ni
mfanyabiashara kutakiwa kulipa ushuru katika Kijiji cha Lwande na
kukataa hivyo mgambo waliingilia kati ndipo wafuasi wao walichukua
uamuzi wa kwenda kuwakata mapanga mgambo ambao mmoja alijeruhiwa na
mwingine kuuawa.
----MAJIRA
----MAJIRA
0 comments:
Post a Comment