Jeshi la Polisi, Wilaya ya Kilindi, mkoani Tanga, limemkamata mfanyabiashara wilayani humo, Bw. Juma Kheri maarufu kwa jina la 'Chifu Abiola', akituhumiwa kufadhili kikundi cha kigaidi kilichokuwa na kambi tatu Kata za Lwande na Negero.
Akizungumza
na Majira, Mjini Songe, Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Suleiman Liwowa
alisema Bw. Kheri alikamatwa siku tatu zilizopita na yupo mahabusu
wilayani Handeni.
Hata hivyo, Bw. Kheri alipekuliwa katika nyumba
anayoishi, duka la jumla na nyumba ya kulala wageni kuanzia 8:30 mchana
hadi saa 12.30 jioni.
Bw. Liwowa alisema polisi walipata shida
kubaini jina lake halisi, kwani alikuwa anatambulika kwa majina ya Juma
Sahel, lakini baadaye wakabaini anaitwa Juma Abdallah Kheri.
"Hadi
sasa bado anashikiliwa polisi Mjini Handeni, watu walikuwa wakimjua kwa
majina mengine lakini hivi sasa jina lake halisi libebainika," alisema
Bw. Liwowa.
Alisema watu wengine wanaohusishwa na vitendo vya ugaidi
wamekamatwa kwenye Kijiji cha Gombero, Kata ya Kibirashi wilayani
humo.
Aliwaomba wakazi wa Wilaya hiyo,wasiwachukie waumini wa
dhehebu la Ansaar Sunna kwani si wahalifu bali waliokuwa wanafanya
vitendo vya kigaidi ndiyo wahalifu.
"Serikali haipambani na Ansaar
Sunna, bali wahalifu, sisi tunaheshimu dini zote hivyo mnapowaona
waumini hao msije mkawafanyia vitendo vibaya," alisema Bw. Liwowa.
Aliongeza
kuwa , awali hawakujua kama kundi lilo ni tishio lakini tangu wameanza
kupambana nalo, wamebaini ukweli na nguvu yao ni kubwa.
Bw. Liwowa
alisema hadi sasa kikundi hicho kimeweza kusambaratishwa lakini polisi
bado wameweka kambi kwenye Kata za Negero na Lwande.
Mbunge wa
Kilindi, Beatrice Shelukindo, alisema kundi hilo ambalo lilikuwa
likifanya vitendo vya ugaidi katika Kata za Lwande na Negero,
lisihusishwe na dini ya Kiislamu bali hao ni magaidi, majasusi na
wanatakiwa kulaaniwa na kupingwa.
"Lile ni kundi la kigaidi si
wahalifu wa kawaida, lakini naomba lisihusishwe na dini ya Kiislamu,
sisi sote tunafahamu hakuna dini inayoruhusu vitendo vya ugaidi,
kuvuruga amani," alisema
CHANZO:MAJIRA.
0 comments:
Post a Comment