DIWANI wa Kiomoni, Masota Mayala (CCM), amefariki
dunia juzi kutokana na maradhi ya mapafu na ubongo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, mtoto
wa marehemu, Kelvin Mayala, alisema kifo cha baba yake kimetokea
ghafla na ni pigo kubwa kwao.
“ Kifo cha baba yetu ni pigo kubwa kwetu na familia
kwa ujumla kwani alikuwa ni nguzo katika maisha yetu,” alisema Mayala.
Alisema baba yao alianza kusumbuliwa na maradhi
hayo tangu mwezi uliopita na alikwenda katika Hospitali ya Masana, iliyopo
Mbezi, Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Tanga, Lusia Mwiru,
alisema kifo hicho ni pigo kubwa kwao na serikali kwa ujumla, kwani diwani
huyo alikuwa ni mwadilifu na mchapa kazi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego alisema
wilaya yake na CCM waimepata pigo kwa kumpoteza diwani huyo ambaye alikuwa
mshauri mkubwa wakati wa kutekeleza ilani ya chama hicho.
Alisema mazishi ya Diwani Mayala yamefanyika jana
katika kata hiyo.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment