JAMII ya watu wenye ulemavu mkoani Tanga wameiomba serikali
kuwatengenezea vitambulisho maalumu vitakavyawawezesha kupata huduma za kijamii
bila manyanyaso kutoka kwa baadhi ya watumishi wa umma wasiojali ulemavu wao.
Hatua
hiyo ya walemavu hao kudai vitambulisho inatokana na miongoni mwao kudai
kutotendewa haki kwenye huduma za matibabu hususani katika vituo vya afya na
daladala ambako wamekuwa wakidharauliwa utu wao.
Kwenye
kikao maalumu cha maandalizi ya rasimu inayohusu huduma za afya kwa watu wenye
ulemavu wajumbe wa kikao hicho pamoja na mambo mengine wamejadili kwa kina
kuhusu mustakabali wa maisha yao katika kupata huduma za kijamii bila kujali
hali zao za ulemavu.
Lakini
katika hali ya kustaajabisha na iliyowaacha midomo wazi wajumbe wa kikao hicho
Mwenyekiti wa Chama cha walemavu mkoani Tanga Zuhura Musa na M/kiti wa chama
hicho taifa Shida Salimu wametofautiana mtizamo na wajumbe hao kuwa
vitambulisho vinazidisha unyanyapaa dhidi yao.
Kwa
upande mwingine Katibu wa Chama cha Albino nchini Ziada Sembu anawataka
walemavu wote bila kujali aina za ulemvu wao kuungana ili kutetea haki haki zao
kwa madai kuwa juhudi hizo zimeanza kuzaa matunda ya kuheshimika kwenye jamii
na kushirikishwa kwenye vyombo vya maamuzi.
0 comments:
Post a Comment