Home » » Serikali yakalia pesa za Ukimwi Tanga

Serikali yakalia pesa za Ukimwi Tanga

MTANDAO wa waratibu wa Ukimwi Kanda ya Kaskazini umesema unakabiliwa na changamoto ya kuchelewa kwa fedha toka serikalini hali ambayo imeelezwa kuchangia kushindwa kufanya vikao vya tathimini kwa wakati kwenye maeneo yao.

Mikoa inayounda mtandao huo ni pamoja na Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga ambapo waratibu wake wamekutana jijini Tanga pamoja na mambo mengine kufanya mkutano wa kutathimini hali ya maambukizi ya VVU/Ukimwi.

Mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo wa siku tano Mtandao huo
ukiongozwa na Mwenyekiti Charles Mtali ulizulu katika kituo cha
kulelea watoto yatima cha Nyumba ya Furaha kinachomilikiwa na Kanisa
Katoliki kilichopo Raskazone jijini Tanga na kutoa misaada mbalimbali
iliyotokana na michango yao.

Moses Kisibo ni Mratibu wa Ukimwi jijini Tanga ambaye pamoja na mambo mengine anabainisha kuwa wameamua kutoa sehemu ya posho yao ya kujikimu kwa ajili ya kuwasaidia watoto wasiokuwa na wazazi.

Baadhi ya masister wa kituo hicho wameushukuru mtandao huo kwa msaada wao kujitoa kwa ajili ya watu wenye mahitaji mbalimbali.

Misaada iliyotolewa na mtandao huo ni pamoja na mafuta ya kula lita
10, katuni tano za sabuni, sukari kilo 20, Mchele kilo 20 na juice
vyote vikiwa na thamani ya shilingi 250,000.

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa