KAMPUNI ya Bia nchini TBL imekabidhi visima 15 vyenye thamani
ya zaidi ya shilingi milioni 40 ilivyochimba katika vijiji vinne vya kata ya
Kwamgwe wilaya ya Handeni mkoani Tanga ikiwa ni sehemu mojawapo ya kutumia
sehemu ya faida yake kwa shughuli za kijamii.
Kukamilika kwa
visima hivyo ni mojawapo ya ahadi ya kampuni hiyo iliyoitoa mwezi Octoba mwaka
jana ambavyo vimechimbwa kwa usimamizi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tanga
kwa msaada wa TBL.
Katika mahojiano
na kituo hiki yaliyofanyika katika kijiji cha Bondo baadhi ya wakazi wa kata
hiyo wameelezea furaha yao sanjari na kuishukuru TBL kwa kukubali kufadhili
uchimbaji wa visima hivyo.
Mkurugenzi wa
Uhusiano na Sheria wa TBL Bw. Steven Kilindo na msimamizi wa mradi huo Padre
Edward Haule kutoka kanisa la Angilikana Dayosisi ya Tanga pamoja na mambo
mengine wamewataka wakazi hao kuutunza badala ya kuhujumu miundombinu yake.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Handeni Ramadhani Diriwa ameishukuru TBL kwa ufadhili
wa mradi huo na kutoa rai kwa wananchi kuutunza ili kampuni hiyo iweze
kutoa ufadhili kwa maeneo mengine.
Takwimu
zinaonyesha kuwa 56% ya wakazi wa wilaya ya Handeni hawapati huduma ya maji
safi na salama licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau wa maendeleo
ikiwemo TBL.
0 comments:
Post a Comment