WAZIRI wa Viwanda na
Biashara Dr. Abdalah Kigoda ameongoza mamia ya wakazi wa wilaya ya Kilindi
mkoani Tanga kwenye mazishi ya aliyekuwa
mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Husein Semdoe kijijini kwao
Mafuleta kata ya Jaila wilaya ya Kilindi aliyefariki April 10 kwa
ajali ya gari wilayani Handeni.
Wakati Dr. Kigoda akiongoza mazishi hayo, wilayani Muheza nako Katibu
tawala wa wilaya Paul Moshi aliongoza mamia ya wakazi wa wilaya hiyo
katika mazishi ya mwandishi mwingine Hamis Bwanga aliyezikwa kijijini
kwao Lusanga.
Dua ya kumwombea marehemu imesomwa na Shehe wa kata hiyo Omar Rajab ambaye pamoja na mambo mengine amewakumbusha wanadamu kuhusu kujiandaa kwa kutenda mema alivyokuwa maremu.
Dr. Kigoda ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni na mkuu wa wilaya
ya Kilindi wamemuelezea marehemu kuwa alikuwa ni mtu wa kujituma
katika kuihudumia jamii kupitia sekta ya habari.
Nao baadhi ya waandishi waliowahi kufanya kazi na marehemu Semdoe
wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habri mkoani Tanga Hassan Hashimu wameelezea jinsi walivyoguswa na msiba huo.
Ajali hiyo ilitokea April 11 mwaka huu ambapo watu watatu wakiwemo
waandishi wa habari wawili Husein Semdoe kutoka gazeti la Mwananchi na
Hamis Bwanga kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo pamoja na Afisa
Uhamiaji wa wilaya ya Handeni Mariamu Husein walipoteza maisha.

0 comments:
Post a Comment