Wizara
ya Ujenzi inapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa Mgeni Rasmi katika
sherehe za ufunguzi wa barabara ya Tanga – Horohoro ambayo imejengwa kwa
kiwango cha lami ikiwa na urefu wa kilomita 65.14. Aidha, sherehe hizo zitahudhuriwa na
Bw. Daniel Wolde Yohannes, Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Changamoto za Milenia wa
Marekani.
Barabara
ya Tanga – Horohoro ni sehemu ya barabara inayoiunganisha Tanzania na nchi
jirani ya Kenya kupitia mkoa wa Tanga. Mradi
huu umepata msaada wa Serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Changamoto za
Milenia (Millennium Challenge Corporation - MCC).
Kukamilika
kwa barabara hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya Nne ya
kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri wa barabara. Aidha, kukamilika kwa barabara hii
kutapanua fursa za kibiashara kati ya Tanzania na Kenya na hivyo kutumia vizuri
zaidi fursa za Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sherehe
hizi zitafanyikia kijiji cha Kisera katika Wilaya ya Nkinga mkoani Tanga.
Taarifa hii imetolewa na;
0 comments:
Post a Comment