na Chalila Kibuda, Handeni
BARAZA
la Watoto wa Kata ya Sindeni, wilayani Handeni, mkoani Tanga wameitaka serikali
kuingilia kati adhabu ya viboko kutokana na walimu kupitiliza viwango na
kuwafanya wanafunzi kusoma kwa woga.
Akizungumza
na Tanzania Daima hivi karibuni, Mwenyekiti wa baraza hilo, Asnath Mbellwa,
alisema adhabu ya viboko katika Kata ya Sindeni imekuwa tishio kwa wanafunzi na
kusababisha kushuka kwa usikivu wakiwa darasani.
Alisema
walimu wameipa adhabu hiyo majina ‘viboko vya supu’ na ‘dua’ na kusema kuwa
haina lengo la kumfundisha mwanafunzi bali kumnyanyasa na kumdhalilisha.
“Viboko
kwetu ndio kilio chetu kwa wanafunzi wa Sindeni na kuwafanya kusoma katika
uwoga ambao mwisho wa siku mwanafunzi anakosa kujiamini,” alisema.
Naye
Kaimu Ofisa Mtendaji, Amina Sikwatu, alisema atafuatilia kwa karibu juu ya
viboko hivyo kwani serikali ilishapiga marufuku.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment