Home » » WATIMULIWA KIKAONI KWA UTOVU WA NIDHAMU

WATIMULIWA KIKAONI KWA UTOVU WA NIDHAMU

na Shehe Semtawa, Muheza
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Ibrahimu Matovu, amewatimua Ofisa Mtendaji wa Kata ya Misalai, Mussa Chubwa na Mwenyekiti wa Chama cha NLD, Athuman Abadallah, kwenye mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC), kutokana na utovu wa nidhamu.
akizungumza na Tanzania Daima mwishoni mwa wiki, mkurugenzi huyo alisema kutimuliwa kwa watendaji hao kumetokana na kuonesha utovu wa nidhamu wakati Mkuu wa wilaya hiyo, Subira Mgalu, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano na watendaji wao, kuhusu maendeleo ya wilaya hiyo.
Matovu alisema wakati mkuu huyo wa wilaya (DC) akijadili agenda mbalimbali muhimu, alibaini watendaji hao walikuwa wakibishana kuhusu kitabu cha mahudhurio ambacho ndiyo ni maalumu kwa ajili ya posho za kikao.
Alisema kutokana na watendaji hao kuendesha mkutano wao usio rasmi, hali hiyo ilimkera na kuwatoa nje ya ukumbi.
Chanzo: Taaanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa