Home » » MATUKIO YA WATU KUUAWA KIKATILI TANGA, POLISI WAHAHA KUDHIBITI VIFO VIFO HIVYO, HOFU YATANDA KWA WAKAZI WA MKOA HUO

MATUKIO YA WATU KUUAWA KIKATILI TANGA, POLISI WAHAHA KUDHIBITI VIFO VIFO HIVYO, HOFU YATANDA KWA WAKAZI WA MKOA HUO

Mwandishi wetu, Tanga Yetu
JESHI la polisi mkoani Tanga limetoa ufafanuzi kuhusiana na vitendo vya mauaji vilivyotokea mwezi uliopita na kusababisha vifo vya watu 11 vilivyotokana na sababu mbalimbali mkoani humo.
Hofu kubwa imetanda miongoni mwa wakazi wa mkoa huo kutokana na vitendo hivyo ikiwemo kutekwa na kupotelea katika mazingira ya kutatanisha hali ambayo imezua hofu na wengine kushindwa kutembea nyakati za usiku.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Bw. Costantine Massawe amewaambia waandishi wa habari ofsini kwake kuwa vifo hivyo vimetokana na sababu mbalimbali ikiwemo, wivu wa kimapenzi, wizi na ulevi.
Amewataja waliopoteza maisha katika kipindi cha siku kumi kuanzia Sept 14 hadi 24 kuwa ni Abdalah Athumani (23) mwendesha bodaboda mkazi wa Tangasisi jijini Tanga, Mwajuma Kishi (31) mkazi wa Chang’ombe Handeni, Rameck Jonas (35).
Wengine ni Kilo Husein mkazi wa Chanika Handeni, Andrew Omar (82) mkazi wa Kwangema Mkinga, Shaban Zuberi (34) mkazi wa Msambweni jijini Tanga, Ali Said (35-40) mkazi wa Kwafungo Muheza, Frida Michael (22) mkazi wa Kwai Lushoto.
Wengine majina yao hayakufahamika mara moja.
Blogzamikoa

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa