Mwandishi
wetu, Tanga Yetu
ZAIDI ya wanafunzi 800 wa shule ya sekondari Eckernforde iliyopo jijini
Tanga wameandamana hadi kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa jiji hilo
wakidai kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yao ikiwemo kutofundishwa kwa zaidi ya
miezi mitano sasa.
Hatua hiyo inafuatia malalamiko
ya wanafunzi waliyoyatoa kwa uongozi wa shule hiyo kushindwa kutatuliwa huku
wengine wakirudishwa nyumbani kwa kushindwa kulipa ada na kukosa vipindi
darasani.
Tanga Yetu imeshuhudia
wanafunzi hao kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne wakirandaranda mitaani
ambapo katika mahojiano wamesema wameamua kudai haki yao kwa maandamano baada
ya utatuzi wa mezani kushindikana.
Hata hivyo msemaji wa taasisi
ya Elimu Eckernforde Bw. Nyero Msagati amekiri kuwepo kwa malalamiko ya
wanafunzi hao na kuahidi kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa
taasisi hiyo Bw. Remency Tarimo amesema kuwa matatizo hayo yatapatiwa ufumbuzi
lakini akawalaumu wanafunzi kwa uamuzi wa kufanya maandamano.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment