Na Rose Chapewa, Aliyekuwa
Tanga
WAKULIMA wa mbogamboga nchini, wameshauriwa kujenga nyumba,
kwa ajili ya kuandaa na kuhifadhia miche ili kuandaa miche bora na kunufaika na
kilimo hicho.
Ushauri huo ulitolewa na Katibu wa Kikundi cha wakulima wa mbogamboga cha Upendo Joyce Mnkanda, wakati wa ziara ya mafunzo, iliyowahusisha wakulima wa mkoani Morogoro chini ya uratibu wa shirika lisolo la kiserikali la Care International, iliyofanyika Wilani Lushoto mkoani Tanga.
Katibu huyo alisema, Mradi huo umewanufaisha wakulima hao kwa kuwa umewafanya watoke kwenye lindi la umasikini na kuongeza kipato, hivyo kuwaweza kusomesha watoto wao kwenye shule zenye kiwango cha kimataifa.
“Kwa kweli ningewaomba muweze kuchanga hizo fedha ndogo mnazozipata kutoka kwa wafadhili wenu, ili muweze kujenga nyumba za kuoteshea mimea, hizi zina faida sana tena sana.
“Hivyo kwa hali hii unaweza kupata fedha nyingi kwa mfano mimi najitegemea mwenyewe nasomesha watoto hadi chuo kikuu,” alisema Mnkanda.
Kwa upande wake Mkuu wa mradi wa kilimo hifadhi kutoka shirika la kimataifa la Care International, Shariff Maalim Hamad, alisema kuwa shirika hili litasaidia wanakundi wao pale walipoishia, ili kuweza kuongeza uzalishaji zaidi.
“Sisi tupo hapa kuwasaidia kuweza kupata mafanikio kwenye kilimo, ila lazima mtu ajisaidie kwanza ndipo aweze kusaidiwa pale alipokwama, kwa hiyo tunapokea ombi lenu na tunasubiri mtuambie mmefikia wapi, ili tuangalie jinsi ya kujazia pale palipopungua,” alisema.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment