Na Mohammed Mhina, Handeni
MKUU wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Muhingo Rweyemamu, amewataka vijana wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo yakiwamo matunda, kujiunga katika vikundi na kuanzisha mashamba ya miti ya matunda.
Alikuwa akizungumza na vijana katika maeneo ya Chanika na Segera mpakani mwa Wilaya za Handeni, Korogwe na Muheza.
Muhingo amesema kama vijana watajiunga katika vikundi na kuanzisha mashamba ya miti ya matunda wataweza kunufaika kwa kuinua vipato vyao na kubadilika maisha.
Kazi ya uchuuzi wa matunda kwa kuyatembeza mikononi haitaweza kuwakomboa katika uchumi kwa vile faida kubwa itaishia kwa wakulima wanakochukua matunda hayo tofauti na kama watakuwa na mashamba yao, alisema.
Alisema kama vijana wataungana na kuanzisha vikundi vya ushirika itakuwa rahisi kwa Serikali kuwapatia huduma ikiwamo mikopo ya kukuza mitaji yao.
Tayari Wilaya ya Handeni imenunua matrekta kwa ajili ya kuwalimia watu mbalimbali wakiwamo vijana wenye vikundi vya ushirika, alisema.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Handeni amewataka vijana hao kuiga mfano wa vijana wenzao wa Kijiji cha Misima wilayani humo ambao wamejiunga pamoja na kuomba kupatiwa eneo la kilimo kutoka Serikali ya Kijiji.
Katika ziara hiyo, Muhingi alifuatana na wataalam mbalimbali wakiwamo maofisa ushirika ambao nao wamekuwa wakitoa elimu za masuala ya ushirika.
Idadi kubwa ya vijana katika Wilaya ya Hendeni wamekuwa wakijishughulisha na biashara ndogondogo zikiwamo za matunda licha ya kuwapo maeneo makubwa ya kilimo.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment