na Bertha Mwambela, Tanga
WAKATI sensa ya watu na makazi ikitarajiwa kuanza kesho kutwa, kumekuwa na tatizo la kukosekana kwa ushirikiano kwa baadhi ya wenyeviti wa mitaa mkoani hapa.
Kauli hiyo ilitolewa na mratibu msaidizi wa sensa Wilaya ya Tanga, Juma Mkombozi, wakati wa kufunga mafunzo ya wasimamizi na makarani wa sensa.
Alisema kumekua na tatizo la baadhi ya wenyeviti wa mitaa kukataa kutoa ushirikiano kwa makarani na wasimamizi wa sensa wakati wa mafunzo yaliofanywa kwa vitendo kwenye mitaa mwishoni mwa wiki iliopita.
“Tunasikitika kuwa kuna changamoto kubwa inatukabili katika zoezi letu ambalo kwa sasa linaelekea mwisho, wenzetu tuliowategemea sana katika kufanikisha kazi yetu wao wamekuwa mstari wa mbele kutuangusha kwa kukataa kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa,” alisema.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Hilda Makwinya, alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa tayari wao kama ofisi wameshapanga ratiba ya kupita katika mitaa na kata kuanzia Augosti 23 mwaka huu, ili waweze kufanya vikao vya ndani na vya hadhara pamoja na wenyeviti hao kuhakikisha wanashiriki vema.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment