Home » » WATAKA KATIBA IZUIE WAGENI KUPEWA LESENI ZA UWINDAJI

WATAKA KATIBA IZUIE WAGENI KUPEWA LESENI ZA UWINDAJI

Nassir Abdul, Muheza.

KATIBA mpya imependekezwa kupiga marufuku utoaji wa leseni za ugawaji wa vitalu vya uwindaji kwa wageni wa kutoka nchi za nje ili kuondosha hatari ya kumalizwa raslimali ya wanyama nchini.

Pendekezo hilo limetolewa na mkazi wa Kijiji cha Zeneti Wilayani hapa, Jumaa Killo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusiana na mchakato unaondelea wa maoni ya katiba mpya.

Amesema utoaji wa leseni za vitalu vya uwindaji wa wanyama umeanza kuhatarisha ustwai wa raslimali hiyo ya Taifa kwa wageni kujinufaisha kwa kutorosha wanyama na kuwapeleka nchi za nje kwa ajili ya kuanzisha mashamba ya maonyesho huku Tanzania ikibaki masikini.

Badala yake amesema kama kuna ulazima wa kupunguza baadhi ya wanyama katika hifadhi zilizopo basi kazi hiyo ifanywe na chombo cha Serikali kwa muda maalumu na madhumuni yaliyolengwa.

Kuhusu muundo wa Muungano, mwanakijiji huyo amependekeza kuwe na Serikali moja yenye bunge moja na wimbo wa Taifa mmoja ikiwa ni hatua muhimu ya kuondosha mgawanyiko ulioanza kujitokeza na kuleta umoja miongoni mwa wananchi wa Tanzania bara na visiwani.

Amependekeza pia unapofikia wakati wa uchaguzi namna ya kupmta Rais isiangaliwe wapi anatoka kati ya Tanzania bara na visiwani bali achaguliwe kutokana na sifa zake kwani licha ya kuleta mgawanyo wa Zanzibar na Tanganyika pia inahatarisha mgawanyo wa kikanda.

Kwa upande wa mgawanyo wa raslimali,amependekeza katiba mpya iwe na kipingele kinachoeleza kwamba raslimali yoyote iwe ni madini,mafuta,gesi ,maji,misitu na mbuga mahala popote itakapokuwa nchini ihesabiwe kuwa ni mali ya Taifa na kwamba mgawanyo uwe sawa.

Blogzamikoa

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa