Na Amina Omari, Muheza
WACHIMBAJI haramu wa madini waliovamia Kata ya Zirai na Misalai, Tarafa ya Amani wilayani Muheza, wamepewa wiki mbili kuondoka. Agizo hilo limetolewa mjini hapa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, alipofanya ziara ya kuhamasisha mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi.
Alisema kuna wachimbaji haramu wamevamia Tarafa hiyo ya Amani, wanachimba madini ambapo sasa wamevamia katika Hifadhi ya Msitu wa Taifa wa Amani wakiharibu mazingira katika msitu huo kwa kuchimba madini.
Alisema wachimbaji hao haramu wanaharibu mazingira, ikiwamo vyanzo vya maji na misitu, kitu ambacho Serikali haitakubali Muheza iwe jangwa.
Alisema Kata ya Misalai wana mtindo wa kuchimba madini haramu katika vyanzo vya maji na kuwataka waache mara moja na kama madini yapo basi wachimbe kwa kufuata sheria.
Alisema kazi hiyo ni ngumu na wanachimba hawapati madini yoyote, bali wanahatarisha ndoa zao kwa kumaliza nguvu katika kuchimba madini na kwamba hataki kabisa kuwaona sehemu hiyo madalali ambao wananunua madini waondoke kabisa hapo.
Kwa upande wake, Ofisa Msitu wa Hifadhi ya Amani, Steven Mmasi, alisema wachimbaji hao haramu wamevamia katika msitu wake, wanaomba ulinzi mkubwa kuwaondoa.
Alisema wachimbaji hao wamevamia msitu huo baada ya kupata taarifa kwamba kuna mtu alikuwa anachimba shimo akapata madini, ndipo na wao wamevamia kwa wingi katika msitu huo.
Alisema wachimbaji hao hapo mwanzo walifukuzwa, lakini wamerudi tena upya wanaharibu mazingira katika msitu huo.
Alisema kwa sasa wakitaka tatizo hilo liishe kunatakiwa kupatikana askari wengi washirikiane na kituo cha polisi kilichopo Amani.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment