Home » » WALAANI HUKUMU YA MGOMO WA WALIMU

WALAANI HUKUMU YA MGOMO WA WALIMU

na Mbaruku Yusuph, Tanga
CHAMA cha wafanyakazi wa migodi, Nishati, Ujenzi na Kazi nyinginezo mkoani Tanga (Tamico), kimelaani taratibu za kisheria zilizochukuliwa na serikali juu ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu ya Divisheni ya Kazi, kusimamisha mgomo wa walimu na kuwataka warejee kazini.
Katibu wa Tamico ambaye pia ni Katibu wa Shirikisho la Wafanyakazi Mkoani Tanga, Ahmed Ngereza alisema, kitendo hicho kilichofanywa na serikali ni kujitetea kwa wananchi ili kulinda maslani yao bila ya kujali madai ya msingi yanayoliliwa na waalimu hao.
Ngereza alisema, bado lengo la kudai maslahi ya walimu hao lipo, vyama vya wafanyakazi vitakuwa imara kama lengo la vyama hivyo lilivyo la kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi wote.
Aliionya serikali kuacha kuonesha nguvu au ubabe ili kukwamisha madai ya msingi yaliyotolewa na walimu ambao wanahaki sawa na wafayakazi wengine hapa nchini.
Alisema, Serikali bado ina nafasi na inaweza kukaa chini na Walimu hao kukubaliana ili walimu nao waweze kuishi na kufanyakazi zao kama wenzao wa sekta nyingine.
Alitoa angalizo kuwa, mgomo huo unaweza kuleta athari mbaya zaidi ikizingatiwa kuwa sekta hiyo ndiyo inayotoa wataalamu wote.
Aliitaka serikali kutatua tatizo hilo ili kuepusha madhara yanayoweza kutolewa.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa