Na Lulu George
Katika hali isiyo ya kawaida watoto wachanga na wenye umri wa chini ya miaka mitano mkoani hapa wamekosa huduma ya chanjo ya ya ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), kutokana na ukosefu wa mabomba ya sindano yanatumika kutoa chanjo hiyo.
Tatizo hilo limejitokeza katika vituo mbalimbali vya afya jijini hapa pamoja na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga ya Bombo.
Hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wakina mama wenye watoto wachanga wanaofika kliniki kwenye vituo vya afya na hospitali ya Bombo, ambapo inawalazimu kurudi nyumbani bila kupata huduma hiyo.
Wakizungumza na NIPASHE jana, wakina mama hao walisema walianza kukosa huduma hiyo katika kituo cha afya cha Makorora kilichopo jijini Tanga, ambapo walielezwa na wahudumu wa afya kufuata huduma hiyo katika hospitali ya Bombo, ambako nako hawakupata huduma hiyo.
“Tulienda Makorora na watoto mgongoni kwa ajili ya kliniki tunaambiwa dawa zipo lakini mabomba ya kuchomea hakuna, tukaambiwa nendeni Bombo tumekuja Bombo tunaambiwa hivyo hivyo sasa tukimbilie wapi”, alihoji Mwanamvua Jumaa mkazi wa Makorora.
Naye Elizabeth Said aliiomba serikali kuongeza umakini katika huduma za afya kwani hali hiyo ni hatari kwa afya za wananchi wake.
“Hivi katika hali ya kawaida mtu akija hospitali anaambiwa hakuna mabomba ya kuchomea BCG mtu huyu kama hana uelewa si ataona chanjo hii haina maana kwa afya ya mtoto wake na unaweza kuwa ndio umemfukuza kabisa asije kumleta mtoto kliniki, sasa nini hatma ya huyu mtoto atakayekuwa bila kinga yeyote tunakuza Taifa la watu gani…inasikitisha”, alisema Said.
Kwa mujibu wa Katibu wa Hospitali ya Bombo, Adam Lyatuu, ni kwamba uhaba huo ni wa nchi nzima na si hospitali ya Bombo tu.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya, kujikinga na Kifua Kikuu kinga ya kuulinda mwili na ugonjwa huo hutolewa kwa watoto wadogo baada ya kuzaliwa.

Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment