Mwanidhi wetu, Tanga
WAKAZI wa kijiji cha Kwamndolwa katika Halmashauri ya mji wa Korogwe wameonyesha wasiwasi wao juu ya zoezi la kuhesabu watu senza wakihofia kusahaulika kutoka na kuishi milimani ambako huduma za jamii kama barabara hazipitiki kirahisi.
Wakazi hao wameitaka halmashauri ya mji huo hiyo kufika maeneo ya milimani wanakoishi kwa kujishughulisha na kilimo ili kutoa elimu kuhusu sensa ya idadi ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Hatua hiyo inafuatia tabia ya halmashauri ya mji wa Korogwe kutopeleka huduma za kijamii mara kwa mara kutokana na ubovu wa miundombinu ya barabara na jiografia ya maeneo hayo kuwa milimani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao wameitaka halmashauri ya mji huo kuhakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi la Sensa ya idadi ya watu na makazi litakapofanyika.
Mjumbe wa kamati ya Sensa katika halmashauri ya mji wa Korogwe Ahmud Mbanza amezungumzia jinsi ya kuwatambua makarani wa zoezi hilo na kutoa rai kwa wananchi kutodanyika na watu wasiowafahamu.
Kwa upande wake Mratibu wa sensa katika halmashauri ya mji huo Grace Mbarouk amewatoa hofu wananchi kwa kuelezea mipango madhubuti ya kutoa elimu na kuyafikia makundi mbalimbali ya kijamii.
Sensa ya idadi ya watu na makazi inatarajiwa kufanyika nchini kote usiku wa kuamkia Agosti 26 mwaka huu ambapo ili kufanikisha azma hiyo watanzania wote bila kujali itikadi za vyama, dini ama kabila wanatakiwa kushiriki kikamilifu.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment