Na Oscar Assenga, Tanga
KAMPUNI na mashirika ya umma mkoani Tanga yametakiwa kuwasaidia Waislamu wasio na uwezo, hasa katika kipindi hiki cha mfungo mtukufu wa Ramadhani.
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Sheikh na Imamu Mkuu wa Msikiti wa Ibadhi Chumbageni, Ally Abdallah, wakati akipokea msaada wa maziwa kutoka Kiwanda cha Tanga Fresh.
Alisema kipindi cha mfungo wa Ramadhani ni wakati muafaka kwa mashirika, kampuni na watu wenye uwezo kujitokeza na kutoa walichonacho kwa watu masikini na kuwawezesha kufunga ikiwa ni pamoja na kufanya ibada nyinginezo.
Alisema ni wakati wa wafanyabiashara kujitokeza na kutoa kila aina ya msaada.
Alizitaka kampuni na mashirika ya umma kuiga mifano ya nchi nyingine ambazo hugawa misaada kwa watu ambao hawana uwezo kila ifikapo Ramadhani.
Alisema ni ukweli kuwa wako waumini wengi wanashindwa kutekeleza ibada hiyo muhimu kutokana na ugumu wa maisha wanayokabiliana nayo.
Kwa upande wake, Ofisa Msaidizi Vyanzo vya Maziwa, Kindamba Namlia, alisema kiwanda chake kimetoa msaada huo ikizingatiwa kipindi chenyewe ambapo pia watumiaji wake wengi ni pamoja na wafungaji.
Alisema kiwanda hicho kitaendelea kuwasaidia Waislamu kadri ya uwezo wake katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani, kwa kuwa mbali ya maziwa kuwa kinywaji pia ni chakula.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment