Na Oscar Assenga, Tanga
MKUU wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, ametangaza utaratibu wa kupita kata hadi kata kuhamasisha wananchi kushiriki mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi, unaotarajiwa kufanyika Agosti 26, mwaka huu.
Kauli hiyo ilitangazwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga, Grace Mwakinya, wakati akifunga mafunzo ya makarani na wasimamizi wa mchakato huo wa Sensa ya Watu na Makazi kwa Jiji la Tanga.
Alisema katika siku chache zilizosalia kabla ya kuanza mchakato huo, atafanya ziara ya mfululizo kupita kata zote 24 za Wilaya ya Tanga, kwa ajili ya kuwafikia wananchi na kuwaeleza umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa sensa.
Aliwataka makarani hao pamoja na wasimamizi wao kuwa waadilifu katika utendaji wa kazi zao watakazozifanya kwa ajili ya kutoa takwimu sahihi zitakazolisaidia Taifa kuweza kupanga mipango ya maendeleo kwa wananchi wake.
Aliwataka wahitimu wa mafunzo hayo kuyatumia vizuri kuliwezesha Taifa kuweza kupata takwimu sahihi na kuwataka watambue dhamana kubwa waliyopewa na Serikali, hivyo hawana budi kufanya kazi hiyo kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu kuwezesha kupatikana takwimu sahihi.
“Naamini mtakuwa waadilifu na uwezo mkubwa katika mchakato wa sensa ya watu na makazi, hasa jukumu hilo zito ambalo mmepewa na Serikali,” alisema Mwakinyo.
Aidha, aliwaomba viongozi wa vyama vya siasa kutoa elimu kwa wananchi pamoja na wanachama wao kuhusu mchakato wa Sensa ya Watu na Makazi.
Kwa upande wake, Mratibu wa Sensa Wilaya ya Tanga, Sabas Kasambala, alisema mafunzo hayo yalianza Agosti 9, mwaka huu na yalishirikisha makarani na wasimamizi 870 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanga.
Alisema wahitimu hao walipatiwa mafunzo ya kutosha kutoka kwa wakufunzi waliobobea katika fani za takwimu na wanachosubiri sasa ni kuanza kwa kazi hiyo usiku wa kuamkia Agosti 26, mwaka huu.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment