Home » » HALAMSHAURI ZATAKIWA KUTUMIA BODI ZA MIKOPO

HALAMSHAURI ZATAKIWA KUTUMIA BODI ZA MIKOPO


na Bertha Mwambela, Tanga
HALMASHAURI nchini zimetakiwa kutoogopa kuitumia Bodi ya Mikopo ya serikali za mitaa kwa kukopa na kupata fedha ambazo zitawasidia kuchochea shughuli za kiuchumi ambazo zimelenga kumnufaisha mwananchi.
Rai hiyo ilitolewa jana na Mjumbe wa Bodi ya Serikali za Mitaa, George Lubeleje alipokuwa akizungumza na wakuu wa idara kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Alikuwa akihamasisha miradi ya kitega uchumi inayoweza kutekelezwa kwa fedha za mkopo toka bodi ya mikopo ya serikali za mitaa.
Alisema, lengo la bodi ni kuhudumia halmashauri nchini kwa lengo la kutoa mikopo nafuu, ili kutekeleza shuguli na miradi ya kiuchumi yenye lengo la kumuongezea kipato mwananchi.
Alisema umuhimu wa bodi hiyo katika halmashauri unatokana na wajibu wa halmshauri katika kujenga na kukarabati miundombinu na kutoa huduma za msingi ili kuchochea shughuli za kiuchumi.
Alisema ni ukweli kuwa, halmashauri haziwezi kutekeleza miradi yake na kuweka vitega uchumi kwa kutegemea fedha zinazotokana na vyanzo vyake tu ambavyo ni kidogo.
“Ninafahamu kuwa fedha zinazotokana na vyanzo vya ndani katika halmashauri nyingi za hapa nchini ni kidogo, hivyo ni wito wangu kwa halmashauri kukubali kukopa kwenye bodi hii ambayo ni chombo chao,” alisisitiza Lubeleje.
Alisema katika kutekeleza jukumu lake la msingi, bodi hiyo imeweza kutoa mikopo kwenye baadhi ya mamlaka za serikali za mitaa na kuzewezesha kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ile ya ujenzi wa masoko, mabasi, majengo ya utawala, uzalishaji umeme, upimaji viwanja, kilimo cha mazao ya tumbaku na zabibu na ununuzi wa zana za ujenzi.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa