Home » » COASTAL UNION KUJIPIMA NA SOFA PAKA

COASTAL UNION KUJIPIMA NA SOFA PAKA


na Mbaruku Yusuph, Tanga
TIMU ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kesho inatarajiwa kushuka kwenye dimba la Mkwakwani jijini hapa kupimana viwango na mabingwa wa zamani wa Kenya, Sofa Paka.
Mwenyekiti wa Coastal Union, Hemed Aurora ‘Mpiganaji’, aliliambia Tanzania Daima kuwa, mechi hiyo ni moja kati ya maandalizi ya timu yake kujiwinda na msimu mpya wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza Septemba mosi mwaka huu.
Aurora alisema, mechi hiyo itakuwa ni ya pili ya majaribio, baada ya awali kucheza na Bandari Mombasa na kulala kwa mabao 3-2.
Alisema, hivi sasa mazungumzo yanaendelea vizuri kati yao na Sofa Paka na yana asilimia kubwa ya mafanikio.
"Tumedhamiria kuhakikisha tunacheza mechi nyingi za majaribio, ili kuweza kukiandaa vema kikosi kwa ajili ya msimu mpya na moto wetu hakuna mtu ambaye anaweza kuuzima,” alisema Aurora.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, Sofa Paka inatarajiwa kutua jijini hapa leo
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa