na Mwandishi wetu
TIMU zaidi ya timu 30 zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Kamanda wa Polisi jijini hapa, Masawe Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema mwezi ujao na kushirikisha wilaya zote za Mkoa wa Tanga.
Mratibu wa mashindano hayo, Sofia Wakati, alisema kuwa, maandalizi yako tayari na alizitaja wilaya ambazo zitashiriki kuwa ni Pangani, Muheza, Korogwe, Lushoto, Handeni, Mkinga, Kilindi na Tanga Mjini.
Aidha, alisema kuwa, lengo hasa la kuandaa mashindano hayo ni kujenga uhusiano mzuri na kuimarisha ushirikiano kati ya polisi na raia.
Alisema, ipo haja sasa kujenga urafiki mwema kwa Jeshi la Polisi na raia kupitia michezo na kuiondoa dhana mbaya ya uadui iliyojengeka muda mrefu na kulifanya jeshi hilo lishindwe kudhibiti vitendo vya uvunjaji wa sheria kwa kukosa ushirikiano mzuri kutoka kwa raia wema.
Aliongeza kuwa, kila wilaya itashindanisha timu katika eneo lake na kutoa timu moja ambayo itashiriki kumpata mshindi kimkoa.
Aliongeza kuwa, mgeni rasmi katika mashindano hayo anatarajiwa kuwa Kamanda wa Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment