Na Mwandishi Wetu, Korogwe
MBUNGE wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani (CCM), amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo, kuwakamata maofisa watendaji wa vijiji, badala ya wenyeviti wa vijiji pindi viongozi hao wanaposhindwa kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi ya vijiji vyao.
Ngonyani ambaye ni maarufu kwa jina la Profesa Maji Marefu, alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mkutano wa kuwahamasisha wenyeviti kuhusiana na Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza nchini kote jana.
Alisema kwamba, kitendo cha kuwakamata wenyeviti wa vijiji na kuwaweka ndani, kinawavunjia heshima yao kisiasa pindi wanaporejea vijijini kwao na kwamba, wanaotakiwa kukamatwa na maofisa watendaji wa vijiji kwa vile ndio wanaotakiwa kuitisha mikutano hiyo.
"Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, zoezi lako lile la kuwakamata wenyeviti wa vijiji pamoja na watendaji wa vijiji kisha unawaweka ndani unawaumiza kisiasa wenyeviti wa vijiji.
“Mimi nakuomba kwamba, badala ya kuwakamata wote ningeomba uwakamate watendaji wa vijiji, maana hawa ndio wanaoshindwa kuitisha mikutano mikuu ya kijiji na hii ni kwa vile wanajifanya ni miungu watu.
“Mimi nakwambia ukianza kuwakamata watendaji wa vijiji, utaona mambo yanabadilika, anza kuwakamata hao kwa sababu ndio wanaokwamisha mambo,” alisema Profesa Maji Marefu.
Mbunge huyo aliyasema hayo baada ya hivi karibuni, Gambo kufanikiwa kuwakamata wenyeviti 138 kutoka katika vijiji 122 vilivyopo Korogwe Vijijini baada ya kushindwa kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi.
Pamoja na mambo mengine, alifikia hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi, kwamba viongozi wao hao hawataki kusoma mapato na matumizi bila sababu za msingi.
Katika hatua nyingine, Profesa Maji Marefu, alisema ataendelea kuibana Serikali ili ianze kuwalipa fedha wenyeviti wa vijiji na wa Serikali za Mitaa na kwamba, jukumu hilo ataanza kulifanyia kazi Bunge lijalo.
"Ninatambua nyinyi mnafanya kazi katika mazingira magumu na pia Serikali inatambua na kuthamini uwepo wanu, nyinyi ni watu muhimu kwani mko karibu na wananchi, nawaombeni mvumilie, mmekuwa na msaada mkubwa kwa Serikali.
“Endeleeni kusimamia vizuri fedha za maendeleo zinazoletwa na Serikali katika maeneo yenu, msidanganyike nawaomba sana," alisema.
Naye Mkuu wa Wilaya, aliwasisitiza wenyeviti hao umuhimu wa kuitisha mikutano ya kisheria kwenye maeneo yao, kwani kitendo chao cha kushindwa kuitisha mikutano hiyo, kinatoa mwanya kwa wananchi kufikiri fedha zao zimetumika vibaya.
"Waheshimiwa wenyeviti niwaombe, chondechonde, muwe mnaitisha mikutano ya kisheria kwenye maeneo yenu na kwenye vikao husika, hakikisheni agenda ya mapato na matumzi haisahauliki, ili kuondoa malalamiko yasiyokuwa na maana," alisema mkuu wa wilaya.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment