Home » » GALLAWA: KILA GARI LIWE NA KITUPIA TAKA

GALLAWA: KILA GARI LIWE NA KITUPIA TAKA

na Bertha Mwambela, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Luteni Mstaafu Chiku Gallawa amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri kuweka vitupia taka katika magari yao kudhibiti hali ya uchafu kwenye barabara zilizopo mkoani hapa.
Gallawa alitoa kauli hiyo ofisini kwake juzi wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usafi mkoani hapa.
“Rai yangu kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri ni kwamba, wakati umefika kwa kila mmiliki wa gari ya abiria kuweka chombo cha kutupia taka ili tuweze kudhibiti uchafu unaotupwa barabarani wakati abiria wakiwa safarini,” alisema.
Alisema yapo matumaini makubwa ya kuweza kubadilisha hali ya usafi mkoani hapa iwapo kila mmoja atatimiza wajibu wake wa kuhakikisha anazingatia kanuni sheria na taratibu za usafi kwa lengo la kutunza mazingira.
Hata hivyo, aliwapongeza wakazi wa Tanga kujitokeza kwa wingi kila Jumamosi ya kwanza ya mwezi kufanya usafi wa mzingira katika makazi na kwenye mifereji inayowazunguka.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa