na Mbaruku Yusuph
VIWANJA vitatu jijini hapa, vinatarajiwa kutumika kwa mashindano ya mpira wa kikapu taifa, Taifa Cup, kuanzia Oktoba 13-21 mwaka huu.
Akizungumza jijini hapa, Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Tanga (TBRA), Hamisi Jaffary, alisema, maamuzi hayo yalipitishwa kwenye kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokutana mwishoni mwa wiki.
Jaffary, alivitaja viwanja ambavyo vitatumika kuwa ni Mkwakwani, Harbors Club na kiwanja kipya kitakachojengwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa zamani.
Aliwataka wapenzi na mashabiki wa mchezo huo, kuyaunga mkono mashindano hayo yatakapoanza, kwa kujitokeza kwa wingi, kwani ni fursa adhimu ambayo wakazi wa Tanga wanaipata msimu huu.
Katika hatua nyingine, aliongeza kuwa chama hicho kitaandaa ligi ya mkoa kuanzia Septemba 3-14 ambayo itatumika kuchagua wachezaji wa kombaini ya mkoa.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment