Na Amina Omari, Muheza
MKUU wa Wilaya ya Muheza, Subira Mgalu, amewapiga marufuku makarani wa sensa wilayani hapa kuvaa nguo ambazo hazina heshima, hasa vimini na suruali za mlegezo.
Mgalu alitoa agizo hilo jana alipowatembelea makarani hao katika semina iliyokuwa ikifanyika katika Shule za Sekondari Mlingano, Bwembwera na Sekondari ya High School.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, zoezi hilo likianza inatakiwa makarani wote kuvaa nguo za heshima na sio kuvaa nguo ambazo ni za kihuni.
Alisema kuwa, hiyo sio tabia nzuri kabisa na kwamba hata yule mtu anayehesabiwa hatafurahia mavazi hayo aliyovaa karani huyo ambaye ameaminiwa na Serikali katika kufanya kazi hiyo ya kuhesabu watu.
Pia Mgalu alitoa onyo kwa makarani ambao watachukua fedha halafu hawatashiriki katika zoezi la sensa na kusema Serikali itawafuatilia ili kuwachukulia hatua..
Alisema kwa mujibu wa sheria namba Moja ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, imeweka wazi hatua mbalimbali za kuchukuliwa endapo kuna haja ya kufanya hivyo.
Alisema kuwa, karani yeyote ambaye ataingiza itikadi za kidini kwa kuandika takwimu za waumini wa dini badala ya kuhesabu watu kwa ujumla wake atakuwa anafanya mañosa.
Mgalu alisema ili kuepusha mgogoro wa aina hiyo ni vema kundi linalopinga zoezi hilo la Sensa, kuandaa utaratibu wao wa kujua idadi ya watu wao kama walivyofanya Wakristo.
Vilevile aliwataka makarani hao kutunza nidhamu pindi zoezi hilo litakapoanza wakienda nyumbani kwa watu kuwahesabu, wawanyenyekee na kuwafundisha mambo ya sensa na sio kuwatukana.
Kwa upande wake Mkufunzi Agness Chilongola, alisema zoezi linakwenda vizuri ingawa hadi sasa mwongozo wa karani wa sensa vikiwemo dodoso refu pamoja na mabegi, havijafika kama ilivyo maeneo mengine.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment