ABIRIA 11 kati ya 12 wamenusurika kufa maji baadaya ya Boti waliyokuwa wakisafiria ijulikanayo kwa jina la MV Salwat kuzama kwa kupigwa na mawimbi yaliyotokana na kuchafuka kwa bahari ya hindi.
Boti hiyo yenye namba za usajili Z 907 ilikuwa ikitokea Mjini Pangani kuelekea Unguja ambapo ilikuwa imebeba abiria 12 waliwamo watalii watatu ambao ni raia kutoka nchi za Ulaya ambazo bado hajijajulikana.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe ni kuwa boti hiyo ilianza kuzama jana jumapili saa 11.00 jioni ilipofika maeneo ya kisiwa cha Maziwe Wilayani Pangani.
Watu walioshuhudia wakati boti hiyo ikijiandaa na safari katika bandari ya Pangani walisema kuwa ilikuwa ikiongozwa na Ahamada Haji Kombo ambaye ndiye mmliki huku nahodha wake akimtahadharisha juu ya
hali mbaya iliyopo baharini.
Alisema hata hivyo nahodha mmiliki wa boti hiyo alitumia mabavu na kuanza safari huku bahari ikiwa imechafuka kutokana na pepo za kaskazi na mvua iliyonyesha siku ya Idd El Fitri mfululizo.
Harakati za kuwaokoa abiria hao zilianza saa 12 jioni baada ya kupiga simu ya kuanza kuzama taratibu kwa boti hiyo ambapo Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Pangani Mashariki, Haji Nundu alifanya jitihada
za kwenda kwenye kituo kimoja na kukopa lita 100 za mafuta ya kutumika kwa boti ndogo za uokoaji.
Hadi saa 6 usiku harakati za uokoaji zilikuwa hazijazaa matunda kutokana na baharini kuwa na giza nene lililotokana na mvua iliyokuwa ikinyesha lakini ilipofika alfajiri, boti za uokoaji kwa kusaidiwa na helkopta ya jeshi la Polisi na ya Jeshi la Wananchi JWTZ ziliweza
kufanikisha kuwaokoa abira 11 wakiwa hai.
Kamanda Massawe amesema alilazimika kupeleka helkopta hizo ili kuongezea nguvu na akasisitiza kwamba jitihada za ziada zinafanyika kumuokoa abiria mmoja ambaye hadi tunaandika habari hizi alikuwa
hajapatikana.
Boti hiyo ina uwezo wa kubeba abiria 35 lakini uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba siku moja kabla ya ajali hiyo iliweza
kuwabeba watu wazima 93 pamoja na watoto 20 na kuwasafirisha kutoka Bandari ya Pangani hadi Unguja.
Blogzamikoa

0 comments:
Post a Comment