na Mbaruku Yusuph, Tanga
TIMU ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ ya jijini hapa, imejivunia usajili wake uliofanywa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara ili kuleta chachu ya upinzani mkoani Tanga ambako kuna timu mbili sasa zilizopo ligi hiyo.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini hapa jana, Mwenyekiti wa Coastal Union, Ahmed Aurora
alisema kuwa, lengo la kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha Coastal Union, ni kurudisha heshima ya soka mkoani Tanga, iliyopotea tangu mwaka 1988.
alisema kuwa, lengo la kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi cha Coastal Union, ni kurudisha heshima ya soka mkoani Tanga, iliyopotea tangu mwaka 1988.
Aurora alisema, kwa kushirikiana na viongozi wenzake, watahakikisha wanajenga timu bora na yenye mafanikiyo mazuri.
Alikiri kwamba, timu nyingi hapa nchini, zinakosa kuwa na ushirikiano mzuri, kitu kinachozifanya zishindwe kupata mafanikio katika msimu mzima wa ligi.
Aliongeza kuwa, wataweka mikakati ya kurudisha imani kwa timu na mashabiki wake katika Mkoa wa Tanga.
“Kikosi kilichoundwa kwa hivi sasa, kitaleta upinzani mkubwa na mabadiliko katika ligi kuu na tunajivunia matunda ya usajili bora uliofanywa kwa timu yetu na tuna uhakika wa kufika katika hatua nzuri katika msimamo wa ligi kama si kutwaa kombe,” alisema..
Aliwaomba mashabiki wa timu hiyo, kujitolea kwa hali na mali na kutoa ushirikiano kwa wachezaji, ili lengo liwe moja tu la kurudisha heshima na upinzani mkubwa kisoka katika Mkoa mzima wa Tanga.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment