Home » » ASHINDWA KUJIUA KWA KUJICHINJA

ASHINDWA KUJIUA KWA KUJICHINJA

na Mbaruku Yusuph, Tanga
MKAZI wa Kata ya Bombani wilayani Muheza, Hamadi Salehe (50) amenusurika kufa baada ya jaribio la kutaka kujichinja na panga nyumbani kwake jana asubuhi kukwama, hilo likiwa ni tukio lake la pili kufanya hivyo.
Kaka wa majeruhi huyo, Zuberi Salehe alisema ndugu yake huyo alipatwa na tatizo la akili baada ya kuugua malaria kwa muda mrefu hali ambayo ilimfanya mara ya kwanza kujichanja chanja na wembe mwili mzima.
Salehe alisema siku ya tukio majeruhi alikuwa anatoka kwa mtoto wa kaka yake kuchukua chakula, alipofika eneo alilokuwa akiishi alifanya kitendo hicho, ndipo alipookolewa na wasamaria wema akiwa ameshajijeruhi sehemu kubwa ya shingo lake.
Alisema baada ya tukio hilo, majeruhi alipelekwa katika hospitali ya wilaya na kupatiwa matibabu katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU).
Naye Muuguzi Msaidizi wa ICU, Angelina Mwakalamale, alithibitisha kupokelewa kwa mgonjwa huyo na kueleza kuwa hali yake bado siyo nzuri hivyo jitihada za kuokoa maisha yake zinaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Constatine Massawe, alieleza kuwa alikiri kuwa hilo si tukio la kwanza kwa mtu huyo, jeshi linaendelea kufanya uchunguzi endapo atapatikana na hatia atafikishwa mahakamani.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa