Kilindi, Tanga
BALAZA la Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga llimekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo kukiuka maagizo ya baraza hilo ya kuwataka wasiendelee na uuzaji wa ardhi bila kufuata kanuni na taratibu zilizopo.
Mbali na hatua hiyo pia baraza limetoa onyo kali kwa baadhi ya wenyeviti na watendaji wa vijiji kuuza ardhi kwa wawekezaji bila kuzingatia mipaka ya madaraka yao na hivyo kuingia kwenye migogoro isiyo na tija.
Kwa mujibu wa sheria ya ardhi No.4 na No.5 ya mwaka 1999 iliyoanza kutumika rasmi mwaka 2001 inawataka wenyeviti na watendaji wa vijiji kuuza mashamba yasiyozidi ukubwa wa ekari 50 lakini imekuwa ni kinyume cha matakwa hayo ya kisheria
Kwenye kikao cha baraza hilo zinaibuka shutuma nzito dhidi ya watendaji wasiokuwa waaminifu ambao wamebainika kuwa chanzo cha migogoro.
Pamoja na lawama hizo kuelekezwa kwa watendaji, madiwani wengine wanasema wao wamekuwa chanzo cha migogoro hiyo kwa kushindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Musa Semdoe pamoja na mambo mengine anasema hati chafu iliyotolewa kwa halmashauri hiyo inatokana na mikataba mibovu ya miradi ya maendeleo iliyosainiwa na wataalamu walioaminiwa.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment