Home » » PPF yaipiga jeki shule ya msingi ya Ubembe, Muheza, Tanga

PPF yaipiga jeki shule ya msingi ya Ubembe, Muheza, Tanga




 Meneja wa mfuko wa pensheni wa  PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akizungumza kabla ya kukabidhi mifuko 50 ya saruji kwa uongozi wa shule ya msingi Ubembe Wilaya ya Muheza kwa ajili ya ujenzi wa darasa la awali shuleni hapo,kulia kwake ni Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Muheza,Peter Jambele na viongozi wa shule hiyo,mifuko hiyo yote ina thamani ya sh 700,000.
 Msimamizi wa mfuko wa pensheni wa  PPF mkoa wa  Tanga,Donald Maeda akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ubembe,Frank Ngulizi mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa la awali la shule hiyo iliyopo Wilayani Muheza linalotarajiwa kugharimu jumla y ash 9,940,000 hadi kukamilika.
  Meneja wa mfuko wa pensheni wa PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ubembe,Hassan Mkebe mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa darasa la awali la shule ya msingi,Ubembe Wilayani Muheza linalotarajiwa kugharimu jumla ya Sh. 9,940,000 hadi kukamilika.
Meneja wa mfuko wa pensheni wa  PPF Kanda ya Kinondoni,Pwani na Tanga,Zahra Kayugwa akiutambulisha rasmi mfuko huo katika kikao cha baraza la madiwani Wilaya ya Muheza,aliyevaa joho ni Diwani wa viti maalumu Tarafa ya Ngomeni,Jestina Mntangi. 
Picha zote na Mdau Fatma Matulanga

0 comments:

Post a Comment

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Tanga Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa